Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Ongeza Muda Unaotumia Kwenye Unachofanya (Time Factor)
ii. Ongeza Bei Ya Unachofanya (Charge Premium Price)
iii. Ongeza Watu Unaowahudumia (Expand Your Client Base)
iv. Idadi Ya Kile Wachonunua (Increase Frequency/Volume Of Sales).
Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia Ya Tatu
– Ongeza Watu Unaowahudumia (Expand Your Client Base)
Hapa unaweka mikakati ya kuwahudumia watu wapya zaidi ya wale uliozoea kuwahudumia. Hii itakulazimu kufanya “marketing” kwenye aina mpya ya watu ambao haujawazoea ili kupata wateja wapya.
Moja ya sababu ya kudumaa kwenye kuingiza pesa ni kuwa na watu walewale hadi soko linakuwa haliwezi kununua zaidi tena (Market Saturation).
Wakati mwingine inawezekana zamani ulikuwa unauza sana kwa sababu ulikuwa peke yako/mlikuwa wachache hivyo ulikuwa unauza kwa faida kubwa, ila kwa sasa mambo yamebadilika sana.
Jaribu kujiuliza, unaweza kufanya nini ili upate watu wapya watakoijua bidhaa/huduma yako zaidi ya wale ambao unao kwa sasa ambao hawanunui zaidi ya unavyotaka?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.