Iran yafanya mazishi ya serikali ya viongozi wa kijeshi waliouawa katika mzozo wa Israel

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g

Majeneza yakiwa kwenye bendera ya Iran, yenye picha za makamanda waliofariki yamezungukwa na umati mkubwa wa watu.

Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Iran kwa takriban watu 60, wakiwemo makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia, waliouawa wakati wa mzozo wa siku 12 na Israel.

Majeneza yaliyokuwa yamefunikwa kwenye bendera ya Iran, yakiwa na picha za makamanda waliofariki yalikuwa yamezungukwa na umati mkubwa wa watu karibu na Enghelab Square katikati mwa Tehran.

Mzozo huo ulimalizika kwa kusitishwa kwa mapigano mapema wiki hii, baada ya Marekani kuhusika moja kwa moja na kulipua maeneo muhimu ya nyuklia nchini Iran.

Miongoni mwa wanaozikwa ni Mohammad Bagheri, afisa wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi nchini Iran ambaye alikuwa mkuu wa majeshi ya Iran.

Umati mkubwa wa waombolezaji waliovalia mavazi meusi wakiimba nara, wakipeperusha bendera za Iran na kushikilia picha za waliouawa.

Mazishi ya Jumamosi yatajumuisha pia Hossein Salami, kamanda mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na wanasayansi kadhaa wa nyuklia kama vile Mohammad Mehdi Tehranchi, ambaye alikuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Azad mjini Tehran.

Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa ”atafikiria” kuishambulia tena Iran.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa BBC Nomia Iqbal katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya White House siku ya Ijumaa, alisema “bila shaka” ataishambulia nchi hiyo ikiwa taarifa za kijasusi zitahitimisha kuwa Iran inaweza kurutubisha madini ya uranium kwa viwango vinavyohusika.

Trump pia amerudia matamshi yake kwamba Iran “imeangamia”, akiandika: “Kwa nini yule anayeitwa ‘Kiongozi Mkuu’ Ayatollah Ali Khamenei, wa nchi iliyokumbwa na vita ya Iran, aseme waziwazi na kwa upumbavu kwamba alishinda vita na Israel, wakati anajua kauli yake ni ya uongo.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment