Maisha ni mshuma uso mkesha.

Kifo kweli hakina huruma. Ajali haina kinga, katikati ya giza totoro,unatuziba na kutupa siku mbaya leo.Nachukua fursa hii kwa masikitiko makubwa kunakili haya,ni swala ambalo limenipata katika majira sikuwazia tukio kama hili linaweza tokea hivi karibuni kwa mpendwa Profesa Ken Walibora jirani eneo la Bonde nyumbani kwao sio mbali sana na kwetu kijijini Makutano kwa ngozi eneo la Cherangany Kitale.

Kifo au mauti hayabishi hodi,Mauti au kifo,kinapotokea ni mwizi asiyebisha hodi.Ajali imetupokonya gwiji wetu Profesa Ken Walibora.Mzaliwa wa Bungoma,lakini familia yake ilinunua,Kipande cha ardhi Cherangany Transnzoia.Kama jamii yeyote ile jamii yangu ilinunua pia ardhi eneo hilo na hapa ujirani ukawa wa sako kwa bako . Unaweza ukachagua marafiki lakini majirani ni Mola anayekuunganisha nao.

Nilienzi uwandishi wake wa vitabu,na usomaji habari wake.

Siku Njema

Hili lilichangia sana,kunikuza,huku mama yangu mzazi alipendezwa na safari kitaaluma , ubunifu na katika uandishi akaomba ushauri kwake,kama ada yake alipenda kushauri “naam mnunulie gazeti la taifa leo na Jumapili na gazeti la nation kila siku na vitabu vya kiswahili”.Avisome hivi nimetaja na atafaulu kiswahili kinalipa.Jambo ambalo mama yangu mzazi alipenda kulifanya pasipo kusita. Mimi kukipenda kiswahili,haikuwa kazi nyepesi ilihitaji malezi ya kina.Kitabu chake cha siku njema nilikienzi na ndicho nilicho tahiniwa katika shule ya upili,ni riwaya ambayo maelezo hayo yananiweka katika taswira ya kubuni picha na mazingara ndani ya mazingira mwandishi anavyo tumia umbuuji wa maneno.

katika ubunifu wake,Sadfa ikawa ni jirani mwema maeneo ya Transnzoia Cherangany,Makutano kwa Ngozi eneo la bonde.Vitabu ambavyo kaka alibahatika kuviandika Sauti ya Mama,Siku Njema, kidagaa kimwozea,Giza totoro, ndoto ya Almasi,kitumbua kimeingia mchanga,Ndoto ya Marikani,Damu Nyeusi,Mayai waziri wa maradhi.

Vitabu hivyo vilinipa chachu kukienzi kiswahili,kuenzi taaluma ya uanahabari na kujitolea kuhifadhi lugha hii na kuitetea.Safari ya kuwa msemaji na mwandishi wa habari kwangu mimi imechangiwa sana na Profesa Ken Walibora.Nilipenda sana kusoma kutoka kwake.Hivi leo ninaviandika vitabu nipo katika hatua ya kuvichapisha.

Cantona Joseph alipokua mwanafunzi alikienzi kiswahili na uandishi wake Profesa Ken Walibora.Kitabu siku njema kiliongeza ladha na chachu yakuwa mtunzi mashahiri swala lililopelekea achapishwe kwenye gazeti taifa leo.

SEHEMU YA PILI. MAISHA NI MSHUMA USIO MKESHA.
Nashukuru Mungu kuniunganisha na Kaka Shisia Wasilwa pale KBC mwaka wa 2003,alinielekeza hadi nikapata fursa ya kujiungaa na Kitengo cha habari cha makamu Rais (VPPS)kutafsiri habari nikiwa mwanafunzi wa taaluma ya habari 2005. Isitoshe vitabu.kadha na makala nimepata fursa kutafsiri kutoka lugha ya kingeeeza hadi kiswahili na kulipwa vizuri kwa kutafsiri vizuri na Kaka yangu Shisia Wasilwa anapopata fursa ya kazi ya kutafsiri.Kiswahili kinalipa na ndicho kimetuweka mjini wengine wetu kwa mda mrefu.

Hatua ambayo imechangia ndoto yangu utotoni kuwa mweledi wa lugha hii.Tajriba niliyo nayo,kuheshimu lugha ya kiswahili inatokana na malezi ya kusoma vitabu na kusikiliza Mwengoya.Ndugu Ken Walibora ni baadhi ya waandishi wa habari na wasomaji habari wachache ambao wanazingatibu za kiswahili andishi na simulizi,Profesa Walibora hakuteleza katika kutunza na kulea lugha ya kiswahili.Alizingatia misamiati na ngeli tangu kipindi akisoma habari KBC,Nation FM,Kabla kuelekea Marekani kwa masomo na baadae kufanya kazi katika chuo kikuu huko akiwa Profesa.Ujio wake tena Kenya na kujiunga na Runinga Q ulinifurahisha maana kizazi hiki kilipata tena fursa kusikiliza tena akitema madini.Kweli si siku Njema tena.Je iwapo Maisha yako ni Kitabu ungekipa kichwa kipi.
Tumepoteza gwiji na mzazi katika jukwa na tasnia ya uandishi wa vitabu na habari.Safiri salama Jirani wangu,eneo letu la Cherangany Makutano kwa Ngozi na Bonde Kitale,tumepoteza shujaa.

Hakika tusigombanie ufito….


Maono aliyokua nayo ambayo amekufa akiwa na tamanio hilo,ni shirika la habari ulimwenguni no shirika la habari ulimwenguni CNN kuanzisha kitengo cha habari za kiswahili.Natumai hili litatimia siku moja na itakua ni siku njema kwa wanahabari wapenzi was lugha ya kiswahili.


Ajali haina kinga safiri salama Jirani Profesa Ken Walibora.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment