Congo yatupilia mbali ombi la kutaka vikosi vya Rwanda kuondoka, vyanzo vyasema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Wapatanishi wa Congo wametupilia mbali ombi la kuwataka wanajeshi wa Rwanda kuondoka mara moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na hivyo kufungua njia ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani kusainiwa kati ya nchi hizo mbili, vyanzo vinne viliiambia Reuters.

Rwanda imetuma takriban wanajeshi 7,000 katika mpaka huo, kwa mujibu wa wachambuzi na wanadiplomasia huku kukiwa na madai kuwa wanaunga mkono waasi wa M23, ambao waliteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Congo na maeneo mengine muhimu mapema mwaka huu.

Hata hivyo, Rwanda imekuwa ikikanusha kuwapa silaha wanajeshi wa M23 na inasema kuwa inajilinda.

Maafisa wa Congo na Rwanda wanatarajiwa kutia saini mkataba wa amani mjini Washington kufuatia msukumo wa kidiplomasia wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kumaliza mzozo wa miaka mingi uliotokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994.

Vyanzo vitatu viliiambia Reuters kwamba makubaliano hayo mapya yanalenga uondoaji wa wanajeshi wa Rwanda kutoka mashariki mwa Congo kwa muda wa miezi kadhaa, huku wawili kati yao wakisema kujiondoa kwao kutatokana na operesheni dhidi ya FDLR.

.

Wanadiplomasia watatu na afisa wa Congo hawakutaka kutajwa kwa sababu mazungumzo hayo ni nyeti.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment