Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi amesema atakuwa “wa kwanza” kupendekeza Rais Donald Trump kupata Tuzo ya Amani ya Nobel ikiwa ataweza kumaliza mzozo kati ya nchi yake na Rwanda.
Katika mahojiano wiki iliyopita na mwandishi wa Ikulu ya White House, Hariana Verás Victória, ambayo yalifayiak Alhamisi, Tshisekedi alisema kuwa Umoja wa Afrika ni ‘moto’, somo alilopata kutokana na vita mashariki mwa nchi yake.
Tshisekedi alisema hayo huku makubaliano ya amani yakitarajiwa kusainiwa Ijumaa hii saa 1:30 jioni mjini Washington – ambayo ni saa 6:30 mchana mjini Kinshasa sawa na saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa DRC na Rwanda.
Vifungu vya kina vya mkataba huu havijulikani, ila vinahusu makubaliano ya kusitisha mapigano, na kutatua wasiwasi wa pande zote mbili katika mzozo wa mashariki mwa DRC.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Trump alijigamba kuwa anafanya mambo makubwa kuleta amani katika sehemu mbalimbali za dunia ambazo ziko kwenye vita, na pia alisema anakwenda kuzikutanisha Rwanda na DR Congo ili kutia saini makubaliano ya amani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.