Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Usiruhusu Ndoto Ifie Ndani Yako.
ii. Usikatishwe Tamaa Unapoona Haupati Matokeo.
iii. Amua Kumchonga Daudi Wako Hata Kama Wamesema Hautaweza.
iv. Jinsi Ya Kujua Kama Haujiamini.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Funzo l
La Pili .
– Usikatishwe Tamaa Unapoona Haupati Matokeo
Wakati nasoma historia ya Brian Tracy moja ya waandishi mahiri sana wa vitabu…
…na mzungumzaji anayelipwa pesa nyingi kwa sasa kuna mambo yalinishangaza sana.
Kwa mara ya kwanza alipoandaa semina kwa ajili ya kufundisha watu…
…anasema alitumia takribani masaa 300 ili kuandaa notisi zake.
Na pia akafanya matangazo sana.
Alikuwa na matumaini ya kujaza ukumbi.
Cha ajabu ni kuwa siku ya semina walitokea watu 7 tu.
Kati ya hao wawili walikuwa ni rafiki yake na mke wake.
Na mwingine ni mdogo wake aliyekuja na mke wake pia.
Hawa wote pamoja na wengine wawili zaidi hawakulipa kabisa.
Mmoja tu ndiye alisema atalipa na ilibidi kumfuatilia kwa miezi 2 hadi alipokuja kulipa dola 295.
Gharama ya semina aliiandaa kwa takribani dola 2000.
Brian Tracy yule yule ambaye watu hawakuwa tayari kumlipa…
…leo hii ameandika vitabu zaidi ya 70 vilivyotafsiriwa kwenye lugha zaidi ya 30.
Na anatafutwa kila kona na kulipwa mamilioni kwa saa moja ya kuzungumza na watu.
Ingekuwaje angesema akate tamaa na aone hawezi tena…
…kwa sababu watu hawajathamini kitu chake?
Sio kila wakati watu wasipoitikia katika unachofanya inamaanisha uache.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.