Mashambulizi ya Israel yawauwa takriban watu 21 huko Gaza, madaktari wanasema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,Mpalestina akikagua eneo la shambulizi la anga la Israeli kwenye nyumba iliyopigwa Jumatano, katika Jiji la Gaza

Milio ya risasi na mashambulio ya anga ya Israel yaliwauwa Wapalestina 21 katika Ukanda wa Gaza siku ya Alhamisi, mamlaka ya afya ya eneo hilo ilisema.

Haya yanajiri wakati wapatanishi wakijaribu kutafuta uwezekano wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo baina ya Israel na Hamas ili kufikia usitishaji mapigano ili kumaliza vita.

Mamlaka za afya za eneo hilo zilisema shambulio la anga la Israel liliua takriban watu tisa katika shule inayohifadhi familia zilizokimbia makazi katika kitongoji cha Sheikh Radwan katika mji wa Gaza, wakati shambulizi jingine likiwauwa watu tisa karibu na kambi ya mahema huko Khan Younis kusini mwa eneo hilo.

Watu wengine watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na Israel na wengine kadhaa kujeruhiwa huku umati wa watu wakisubiri lori za misaada za Umoja wa Mataifa kwenye njia kuu katikati mwa Gaza, madaktari walisema, ikiwa ni tukio la hivi punde zaidi katika msururu wa vifo vingi katika vituo vya kusambaza misaada.

Hakukuwa na maoni ya haraka kutoka kwa jeshi la Israeli juu ya matukio haya.

Israel inasema inataka kuwamaliza wanamgambo wa Hamas, ambao walishambulia kusini mwa Israel kutoka Gaza mwaka 2023, na kuwarejesha nyumbani mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi hilo.

Vifo hivyo vipya vimetokea wakati wapatanishi wa kiarabu, Misri na Qatar, wanaoungwa mkono na Marekani, walifikia pande zinazozozana katika nia ya kufanya mazungumzo mapya ya kusitisha mapigano, lakini hakuna muda kamili uliowekwa kwa duru mpya, kwa mujibu wa vyanzo vya Hamas.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment