Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya ndani wa Kenya Kipchumba anasema kuwa maandamano yaliyofanyika katika maeneo tofauti nchini hapo jana yalikuwa jaribio la mapinduzi.
”Polisi jana hawakutumia nguvu kupita kiasi bali… walizima jaribio la mapinduzi,” alisema Waziri Murkomen akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita.
Aliongeza kuwa hali ambayo maafisa wa usalama walikumbana nayo hapo jana haikuhusiana kwa kwa vyovyote na juhudi za kuwatafutia haki watu ambao waliwapoteza wapendwa wao katika maadamano ya Gen Z ya mwaka jana.
”Maandamano hayo yalichochewa na baadhi ya wanasiasa wanaotumia vijana vibaya kwa lengo la kutaka kuipinduwa serikali,”alisema.
Morkomen pia amesema vituo 9 vya polisi vilishambuliwa katika maandamano ya jana huku vituo vitano vikitetezwa moto na bunduki 5 kuibwa katika sehemu tofauti nchini.
Waziri huyo aidha aliitetea uamuzi wa serikali ya Kenya kufunga mitambo ya matangazo ya mubashara ya maandamano hayo katika vituo viwili vya runinga nchini Kenya akisema walichochea maandamano hayo kwa kuwaelekeza vijana njia ya kufikia ikulu.
Wakati huo huo Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja amesema zaidi ya maafisa 300 wa polisi walijeruhiwa vibaya katika maandamanao hayo.
Kanja ametoa onyo kwa wahalifu waliohusika katika maandamano ya jana kuwa watasakwa na kukamatwa kabla ya kufunguliwa mashataka.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.