Trump apinga shutuma dhidi ya Netanyahu na kuahidi Marekani ‘itamuokoa’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maelezo ya picha,Rais Donald wa Marekani Trump aalipokutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House huko Washington, DC, Marekani, Aprili 7, 2025.

Rais wa Marekani Jumatano alitoa wito kwa Israeli “kufuta mara moja” kesi ya ufisadi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, akielezea kesi dhidi ya “shujaa” kama “hujuma.”

Katika ujumbe mrefu uliochapishwa kwenye jukwaa lake la mitandao ya kijamii la wa Truth Social Trump aliandika, “Kampeni ya mateso kama hii dhidi ya mtu ambaye amefanya mengi ni ya kushangaza kwangu.”

Trump anaamini Netanyahu “anastahili kutendewa mambo bora zaidi, na pia Jimbo la Israel. Kesi ya Bwana Netanyahu lazima iondolewe mara moja au shujaa mkuu asamehewe.”

Chapisho hili linakuja baada ya Trump kufanikiwa kushawishi usitishaji mapigano kati ya Israeli na Iran.

Trump, ambaye anajiona kuwa muathirika wa “hujuma” baada ya kukabiliwa na mfululizo wa mashtaka ya jinai na hukumu ambazo anasisitiza kuwa zinachochewa kisiasa, alisema katika chapisho lake, “Nimefahamu tu kwamba Bwana Netanyahu alifikishwa mahakamani Jumatatu.”

“Mimi na Natanyahu tumepitia kuzimu, tukipigana na adui mkuu wa muda mrefu wa Israel , Iran, na aliweza kuwa bora, mkali zaidi, na mwenye nguvu zaidi katika upendo wake kwa Nchi Takatifu ya ajabu,” aliongeza.

Kesi ya Netanyahu imeahirishwa mara kadhaa tangu ilipoanza Mei 2020, huku mawakili wa waziri mkuu wakiomba kucheleweshwa kwa kwesi hiyo kwasababu ya vita vya Gaza dhidi ya Hamas—na baadaye kutokana na vita dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon, AFP inaripoti.

Katika kesi ya kwanza, Netanyahu na mkewe, Sara, wanatuhumiwa kukubali zawadi za kifahari, kama vile sigara, vito vya mapambo, na champani, zenye thamani ya zaidi ya $260,000, kutoka kwa watu matajiri ili kuwapendelea kisiasa.

Netanyahu pia anachunguzwa katika kesi zingine mbili, akishtumiwa kwa kushawishi utangaza wa taarifa nzuri kumhusu zaidi katika vyombo vya habari vya Israeli.

Netanyahu anakana kufanya makosa yoyote.

Katika chapisho lake, Trump alikumbuka msaada wa kijeshi ambao nchi yake ilitoa kwa Israeli dhidi ya Iran, akisema, “Marekani iliiokoa Israel, na sasa Marekani itamuokoa Netanyahu.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment