Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA amesema mashambulizi ya Marekani “yaliharibu vibaya” vituo vya nyuklia vya Iran na kurudisha mpango huo nyuma kwa miaka mingi, tofauti na ripoti ya kijasusi iliyovuja ambayo ilimkasirisha Rais Donald Trump kwa kutilia shaka uharibifu uliotokana na uvamizi huo.
John Ratcliffe, mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani, alisema maeneo muhimu yameharibiwa, ingawa hakutangaza kuwa mpango wa nyuklia wa Iran umesambaratishwa moja kwa moja.
Hatua hii inatokea siku moja baada ya tathmini ya awali iliyovuja kutoka shirika la kijasusi la Marekani kupendekeza kuwa vituo muhimu vya mpango wa nyuklia wa Iran bado vipo vile vile baada ya mashambulizi.
Rais Trump aliendelea kushikilia kuwa uvamizi huo “umeharibu kabisa” vituo vya nyuklia vya Iran.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.