Wapatanishi wa Gaza wazidisha juhudi za kusitisha mapigano, afisa wa Hamas asema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Afisa mkuu wa Hamas ameiambia BBC kwamba wapatanishi wamezidisha juhudi zao za kufikia makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka huko Gaza, lakini mazungumzo na Israel bado yamekwama.

Hayo yamejitokeza huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema “hatua kubwa imepigwa” tangu Israel na Iran zilipomaliza vita vyao vya siku 12 siku ya Jumanne, na kwamba mjumbe wake Steve Witkoff alifikiria kuwa makubaliano kati ya Israel na Hamas yalikuwa “yanakaribia”.

Mashambulizi ya Israel kote Gaza siku ya Jumatano yaliwauwa Wapalestina 45, wakiwemo baadhi ya waliokuwa wakitafuta msaada, wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas ilisema.

Wakati huo huo, jeshi la Israel lilitangaza kuwa wanajeshi saba waliuawa katika shambulio la bomu siku ya Jumanne.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Brussels siku ya Jumatano, Rais Trump alizungumzia mzozo wa Gaza.

“Nadhani tutakuwa na habari njema. Nilikuwa nikizungumza na Steve Witkoff… [na] aliniambia kuwa Gaza iko karibu sana” kufikia makubaliano, aliongeza.

Muda mfupi baada ya Trump kuzungumza, afisa mkuu wa Hamas aliambia BBC kwamba wapatanishi “walikuwa wanafanya majadiliano ya kina yaliyolenga kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment