Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakiimba “Ruto lazima aondoke,” maelfu ya waandamanaji wamefurika katika mitaa ya Nairobi kumtaka rais ajiuzulu.
Walipeperusha bendera za Kenya na kubeba matawi kama ishara ya upinzani wa amani.
Polisi wameweka vizuizi na waya kuziba barabara kuu – hasusan zile zinazoelekea Ikulu, makazi rasmi ya Rais Ruto na bunge.
Umati wa watu wanasonga kwa vikundi kupitia eneo la katikati mwa mji wa Nairobi. Katika baadhi ya nyakati zisizotarajiwa huku kukiwa na hali ya wasiwasi, waandamanaji walisimama kucheza kandanda kwenye barabara iliyofungwa.
Lakini katika maeneo mengine kadhaa, hali ilibadilika haraka.
Polisi walitumia maji ya kuwasha na mabomu ya kutoa machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wakifurika.
Kanda za video kutoka kwa waandishi wa habari wa kujitegemea zilionyesha moshi mweupe wa mabomu ya kutoa machozi yukifuka kati ya majengo marefu, yna kusababisha waandamaji kukimbia huku wakikohoa na baadhi kumwagia maji nyuso zao kuepuka muwasho wa macho yao. Hatahivyo walionekana wakirudi na kuimba kwa dharau.
Katikati ya jiji la Nairobi, waandamanaji waliandamana kupita maduka yaliyofungwa na barabara tupu. Uzio wa waya wa nyembe kuzunguka bunge uliwekwa kama ukumbusho wa ghasia za mwaka jana, wakati waandamanaji walipokiuka usalama na kuvamia jengo hilo, na kuchoma moto sehemu yake.
Leo, uzio wa bunge ulikuwa umejaa shada za maua na ujumbe wa vijikaratasi vilivyoandikwa kwa mkono kutoka kwa familia zilizoomboleza.
Kulikuwa na mwanamke mwenye umri mdogo aliyevikwa bendera ya Kenya akiwa ameshika bango lililokuwa na majina ya waliouawa mwaka mmoja uliopita na vikosi vya usalama walipokuwa wakijaribu kusitisha maandamano hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.