Tabia Tatu Za Watu Wanaofanikiwa…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kuwa namalengo yaliyoandikwa kila siku
ii. Weka vipaumbele vya Orodha yako
iii. Anza na jambo la muhimu zaidi

Katika Makala Hii Tutazungumzia Tabia Ya kwanza

– Kuwa namalengo yaliyoandikwa kila siku

Bila kujali unafanya shughuli gani, kila siku yako lazima iwe imepangwa na mambo yote uliyokusudia kuyafanya kwa siku husika ni lazima yajulikane.

Inashauriwa kuyaandaa malengo yako usiku kabla asubuhi haijafika, ila kama ukijikuta asubuhi imeshafika na hukuyaandaa usiku wake basi kiwe ni kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kufanya.

Leo, hakikisha unaandika malengo/majukumu yako yote unayotakiwa kuyafanya kwa siku nzima.

Utaalamu unaonyesha kuwa kwa kila dakika moja unayoitumia kujiandaa unaokoa dakika 10 katika utekelezaji.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment