Funguo 5 Unazoweza Kutumia Ili Kuharakisha Maono Yako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Jitambue Wewe Ni Nani Mbele Za Mungu

ii. Wekeza Katika Maarifa

iii. Kuwa Mtatuzi Wa Matatizo

iv. Uwe Mwenye Bidii

v. Uwe Mtu Wa Kuchukua Hatua

Katiba Makala Hii Tutazungumzia Funguo Ya Pili

– Wekeza Katika Maarifa

Moja ya kitu Yesu aliahidi ni kutupatia funguo za ufalme (Mathayo 16:19).

Ili asituache tukiwa hatujui kabisa funguo hizo za ufalme ni kitu gani, ndio maana akasema kuwa MAARIFA ni moja ya funguo hizo ambazo hautakiwi kabisa kuzipoteza (Luka 11:52).

Ili uharakishe kutimiza maono yako ni lazima uwekeze kwenye maarifa.

Ili kufanikisha wito na maono ambayo Mungu alikuwa amemwekea Timotheo, basi ilibidi Paulo amwambie jambo la muhimu la kufanya bila kuchelewa.

Akamwambia “Study to show yourself” (2Timotheo 2:15), akimaanisha, kama unataka dunia ikujue basi inabidi uongeze maarifa kwa bidii.

Hata kama una maono makubwa kiwango gani, kama hauwekezi katika kutafuta maarifa, itakuwa ngumu kwako kuyatimiza.

Kuna mambo mengi sana ambayo Mungu anataka kufanya na wewe ila ni lazima uwe katika kiwango fulani cha maarifa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment