Iran yakanusha madai ya Israel ya kukiuka makubaliano ya usitishaji mapigano – ripoti

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mzozo wa Iran na Israel umesheheni matukio kadh awa kadha katika saa chache zilizopita. Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi haya ndio yaliyojiri kwa ufupi:

Saa Kumi na dakika nane: Donald Trump aliweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wa Truth Social kwamba usitishaji wa vita kati ya Iran na Israel umeanza kutekelezwa.

Zaidi ya saa moja baadaye, Israel ilisema kuwa imekubali pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano,Iran ikisema hapo awali kuwa itasit kushambulia ikiwa Israel itafanya vivyo hivyo.

Saa mbili na nusu: Jeshi la Israel lilisema kuwa limegundua makombora yaliyorushwa kutoka Iran na kuyazuia kaskazini mwa Israeli.

Iran imekanusha kurusha makombora yoyote, lakini IDF inasisitiza Israel “itajibu kwa nguvu”

Kabla ya kuanza kwa mapatani hayo, pande zote mbili zilishambuliana usiku kucha Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vinasema msururu wa makombora kutoka Israel yamepiga mji mkuu na miji mingine – takriban watu tisa wameuawa, akiwemo mwanasayansi wa nyuklia.

Baadhi ya wakazi waliiambia BBC Idhaa ya Kiajemi kwamba waliona mojawapo ya makombora “mizito” tangu mzozo huo uanze siku 12 zilizopita.

Huko Israel, takriban watu wanne wameuawa na 22 kujeruhiwa huko Beersheba.

Tehran ilionekana kuwa tulivu mapema ybaada ya usitishaji mapigano
Maelezo ya picha,Tehran ilionekana kuwa tulivu mapema ybaada ya usitishaji mapigano
Watu wakiwa katika ufuo wa bahari nchini Israel kufuatia tangazo la Donald Trump la kusitisha mapigano
Maelezo ya picha,Watu wakiwa katika ufuo wa bahari nchini Israel kufuatia tangazo la Donald Trump la kusitisha mapigano

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment