Trump aitaka Israel kutoendelea na mashambulizi yake dhidi ya Iran

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Israel kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kutoendelea na mashambulizi yake dhidi ya Iran.

Ujumbe wa Rais Trump ulisomeka: “ISRAEL. MSIDONDOSHE HAYO MABOMU. HATUA HIYO ITAKUWA UKIUKAJI MKUBWA WA MAMLAKA. WAAMBIE MARUBANI WARUDI NYUMBANI, SASA!” Onyo hilo linakuja baada ya Trump kutangaza mapatano kati ya Iran na Israel, ambayo yalianza kutekelezwa mapema leo asubuhi.

Israel ilisema kuwa imekubaliana na pendekezo hilo, huku Iran ikisema itasitisha mashambulizi pale Israel itakapofanya hivyo.

Jeshi la Israel baadaye lilisema kuwa limenasa kombora lililorushwa na Iran.

Tehran ilikanusha kufanya mashambulizi mapya.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment