Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Rwanda limesema kuwa kauli iliyodai kuwa afya ya Rais Paul Kagame iko “hatarini sana” ni Habari za Uongo.
Kauli hiyo ambayo haijafahamika asili yake, imekuja baada ya taarifa mbalimbali kuibuka kuhusu afya ya Rais Kagame baada ya kutoonekana hadharani kwa takribani wiki tatu.
David Himbara, kiongozi wa upinzani anayeishi uhamishoni na mshauri wa zamani wa masuala ya kiuchumi wa Kagame hivi karibuni amekuwa akidai kuwa Rais Kagame ni mgonjwa, na kwamba yuko Ujerumani.
Gazeti la Rwanda la Taarifa lilimnukuu msemaji wa serikali Yolande Makolo akisema kuwa Rais Kagame ni binadamu kama kila mtu, ambaye huchukua muda kupumzika.
Gazeti hilo linamnukuu Makolo akisema: “Rais yuko vizuri na anapumzika kawaida.” Kutoonekana kwa Rais Kagame hivi majuzi kumetolewa maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii na katika mazungumzo ya faragha.
BBC imejaribu kuwasiliana na ofisi ya Rais kuhusu madai hayo, lakini hadi sasa haijafaulu.
Wakati wengi wakiendelea kuhoji madai hayo, jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali taarifa hiyo na kusema ni ‘habari ya uongo’
Rais Kagame alionekana hadharani kwa mara ya mwisho tarehe 6 mwezi huu alipokaribisha kikundi kutoka Shule ya Hope Haven Christian School mjini Kigali, Rwanda.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.