Mkuu wa majeshi ya Uganda awatishia wapiganaji wa Wazalendo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenreali Muhoozi Kainerugaba ameamsha hasira ya wapiganaji wazalendo ambapo amechapisha katika mtandao wake wa X nia yake ya kuwalenga wapiganaji hao, ambao ni washirika wa FARDC katika maeneo kadhaa ya mashariki.

Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenreali Muhoozi Kainerugaba
Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenreali Muhoozi Kainerugaba REUTERS – Abubaker Lubowa

Matamshi yake yanajiri ikiwa imepita siku moja baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano unaolenga kuendeleza operesheni ya pamoja kati ya jeshi la serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC-na lile la Uganda UPDF.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba anadai kuwa Wazalendo wanashambulia raia wa Uganda katika maeneo ya mpakani ambako wanajeshi wa UPDF hawapo, na katika mtandao wake wa X amefahamisha kuwa “hatasubiri” kuwakabili, huku akitoa wito kwa wapiganaji hao kujisalimisha.

Hata hivyo taarifa kutoka eneo la mpaka lililotajwa na mkuu huyo wa majeshi ya Uganda zinasema hakuna matukio yoyote yanayowahusisha moja kwa moja Wazalendo kuwaudhi wala kuwashambulia raia wa Uganda katika siku za hivi karibuni.

Shambulio pekee lililoripotiwa ni la miezi kadhaa iliyopita, eneo la Lubero Mkoa wa Kivu kaskazini ambako kulingana na vyanzo vya kijeshi, shambulio la kuvizia lililohusishwa na watu waliotambuliwa kama Wazalendo liligharimu maisha ya wanajeshi wanne wa Uganda.

Wapiganaji wazalendo wamekasirishwa na kauli hiyo ya jenerali Kainerugaba, wakimtaka kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuathiri mkataba wa kijeshi uliosainiwa jijini Kinshasa hivi karibuni kati ya FARDC na UPDF. Miongoni mwa vitendo ikiwa ni kumkosoa hadharani gavana wa kijeshi wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, akitaka ajiuzulu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment