Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi, ameweka ujumbe hivi karibuni kwenye mtandao wa X akisema kwamba ikiwa Israel itaacha “uchokozi usio halali” Iran “haina nia ya kuendelea kujibu”.
Araghchi alisema Israel lazima isitishe mapigano ifikapo 04:00 saa za eneo, ambayo imepita:
“Kama Iran ambavyo imerudia kusema wazi: Israel ndio ilianzisha vita dhidi ya Iran, na si kinyume chake.
“Hadi kufikia sasa hakuna “makubaliano” juu ya usitishaji vita au operesheni za kijeshi. Hata hivyo, ili mradi utawala wa Israel utasitisha uchokozi wake usio halali dhidi ya watu wa Iran kabla ya saa kumi asubuhi kwa saa za Tehran, hatuna nia ya kuendelea kumjibu.
“Uamuzi wa mwisho juu ya kusitishwa kwa operesheni zetu za kijeshi utatolewa baadaye.
Awali, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza usitishaji “kabisa” wa mapigano kati ya Israel na Iran kwenye mitandao ya kijamii.
Trump alisema usitishaji mapigano utaanza “katika takriban saa sita kutoka sasa” baada ya kila nchi “kupunguza” operesheni zao za kijeshi.
Tangazo la Trump ni njia anayotumia mara kwa mara kupunguza uhasama lakini aliongeza kwamba “ndani ya saa 24” vita vitamalizika rasmi.
Israel yalalamika Iran inaendelea kuishambulia

Tumepokea taarifa kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Israeli, ambalo linasema kuwa Iran imerusha makombora mengine kadhaa kuelekea Israeli.
Taarifa zinasema kuwa mifumo ya ulinzi ya Israel inafanya kazi kuzuia makombora hayo, na kwamba raia wamelazimika kukimbilia makazi ya kujilinda dhidi ya makombora.
Kikosi cha zima moto cha Israel kimesema watu watnne waliuawa katika mashambulizi kusini mwa nchi hiyo huku 22 wakijeruhiwa
Afisa wa Huduma za dharura za Israeli, Magen David Adom, alielezea tukio hilo: “Tuliona moshi mzito ukipanda kutoka eneo la athari, na tulipokaribia, tuliona uharibifu mkubwa kwa majengo kadhaa.
“Nje ya jengo moja tulimwona mwanaume akiwa amepoteza fahamu mlangoni, tulipoingia ndani kufanya upekuzi tulimkuta mwanaume na mwanamke wakiwa wamepoteza fahamu, tukaweka kituo cha kuwahudumia majeruhi na tunawafanyia uchunguzi wa kimatibabu wakazi wanaotoka nje ya majengo hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.