Tunachojua na tusichokijua kufikia sasa kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Katika saa chache zilizopita, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kusitisha mapigano kati ya Iran na Israel – lakini hakuna upande uliothibitisha hadharani wakati huo.

Kisha muda mfupi uliopita, Iran ilisema kwamba ingesimamisha mashambulizi tu ikiwa Israeli ingeanza kufanya hivyo.

Bado hatujasikia kutoka kwa Israeli. Kwa hivyo mambo yanabaki kutokuwa na uhakika.

Tunachojua:

Takriban saa 20:00 kwa saa za huko Qatar (18:00 BST), Iran ilianzisha mashambulizi ikilenga kambi ya Marekani huko Qatar – hakuna hasara iliyoripotiwa.

Saa kadhaa baadaye, Trump alitangaza kusitisha mapigano kati ya Iran na Israel kwenye mitandao ya kijamii, akisema pande zote mbili zitasimamisha mashambulizi yote ndani ya saa 24.

Mashambulio yanaendelea kati ya Iran na Israel, huku kukiwa na ripoti za milipuko mjini Tehran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anasema ikiwa Israel itasimamisha mashambulizi yake ifikapo saa 04:00 kwa saa za huko, haitafyatua risasi.

Kwa sasa ni baada tu ya saa 4:30 mjini Tehran.

Nini hatujui:

Israel haijajibu rasmi madai kwamba pande zote mbili zitaacha mapigano ndani ya saa 24 zijazo

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment