Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Nidhamu ya kihisia
ii. Nidhamu ya kifedha
iii. Nidhamu ya kujiendeleza
iv. Nidhamu ya kuhusiana na watu
v. Nidhamu ya muda
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Kwanza ya Nidhamu Binafsi
– Nidhamu ya Kihisia
Kama hauwezi kujinidhamisha kuhusiana na hisia zako basi utapoteza hatima yako.
Kuna watu wengi wangeweza kuwa wakubwa ila wameshindwa kudhibiti hisia zao katika mapenzi, kula n.k kwa sababu hiyo wameharibu hatima zao.
Sio kila ambacho hisia zako zinakitamani basi unatakiwa kukipata, vingine unatakiwa kujizuia.
Moja ya kanuni kubwa na muhimu kwenye maisha ni ile inayoitwa “The Principle of Delayed Gratification”.
Kanuni hii inakutaka kujizuia mambo yanayokupa raha kwa muda mfupi ili ujijenge kwa ajili ya mambo yatakayokupa faida kwa mudamrefu.
Watu ambao wameshindwa kudhibiti hisia zao, wamejikuta wakiingia katika kufurahia mambo wakiwa chuoni ila yamewaletea madhara baada ya kutoka chuo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.