Hasara 3 za Kutofanya Maamuzi…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Utakuwa ni mtu ambaye kila wakati una msongo wa mawazo katika maisha yako

ii. Utajikuta unadumaa (stagnation) katika hali moja kwa muda mrefu sana.

iii. Kukosa fursa muhimu katika maisha.

Katika Makala Hii Tutazungumzia Hasara Ya Pili

– Utajikuta unadumaa (stagnation) katika hali moja kwa muda mrefu sana.

Mara nyingi tabia ya kutofanya maamuzi imewasababishia watu wengi sana kujikuta wanabakia katika hali fulani kwa muda mrefu bila kupiga hatua inayotakiwa.

Kumbuka kuwa hakuna mwelekeo mpya wa maisha bila kuwa na maamuzi mapya.

Ili uweze kutoka katika hali fulani ambayo imedumu kwa muda mrefu katika maisha yako na uweze kwenda katika kiwango kingine, ni lazima uwe mtu ambaye unafanya maamuzi bila woga wowote.

Kama unataka kuondoka kwenye umaskini ni lazima ufanye maamuzi, kama unataka kuongeza kipato ni lazima ufanye maamuzi.

Kama unataka Kujifunza Zaidi Mbinu Za MAFANIKIO, Nashauri Usome eBook yangu ya TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment