Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kenya imechukua hatua madhubuti za udhibiti wa dawa za kuwaua wadudu kwenye mimea, na kuondoa bidhaa 77 katika soko la Kenya pamoja na kuzuia matumizi ya bidhaa 202 kwa mazao mbali mbali.
Haya yanajiri huku bidhaa zingine 151 zikiwa bado zinakaguliwa na bodi ya kudhibiti dawa za kuwaua wadudu PCPB, kwa mujibu wa wizara ya kilimo na mifugo nchini Kenya.
Uamuzi wa kuidhinishwa kwa bidhaa hizi unatarajiwa kutolewa ifikiapo mwezi Desemba 2025.
Wizara ya kilimo na Mifugo nchini Kenya vile vile imechukua hatua zifuatazo: –
- Bidhaa zote za kudhibiti wadudu (PCPs) zinazozingatiwa kusajiliwa nchini Kenya lazima zisajiliwe katika nchi zilizotoka.
- Hakuna bidhaa za kudhibiti wadudu zilizopigwa marufuku katika kiwango vya kimataifa chini ya makubaliano ya kimataifa ya mazingira zitasajiliwa au kuruhusiwa kwa matumizi nchini Kenya.
- Uingizaji wa molekuli yoyote inayokaguliwa ambayo haijaidhinishwa katika Umoja wa Ulaya, Marekani, Australia, au Kanada itapigwa marufuku hadi kukamilika kwa kukaguliwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.