Marekani yaitaka China kuizuia Iran kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio ameitaka China kuizuia Iran kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi ya meli duniani.

Ametoa maoni yake baada ya televisheni ya taifa ya Iran Press TV kuripoti kuwa bunge limeidhinisha mpango wa kufunga Mlango Bahari huo lakini likaongeza kuwa uamuzi wa mwisho ni wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa.

Usumbufu wowote wa usambazaji wa mafuta unaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi. China haswa ndiyo mnunuzi mkubwa zaidi wa mafuta ya Iran duniani na ina uhusiano wa karibu na Tehran.

Bei ya mafuta ilipanda kufuatia mashambulizi ya Marekani kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran, huku bei ya mafuta ghafi ikifikia kiwango chake cha juu zaidi katika muda wa miezi mitano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment