Mambo 4 Ya Kuepuka Unapokuwa Na Stress Ili Uwe Salama…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Epuka kuamini kwamba hakuna suluhisho.

ii. Usiamini kwamba kila mtu hafai.

iii. Usikubali kubaki mpweke.

iv. Usiache kuchukua hatua.

Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo la Pili

– Usiamini kwamba kila mtu hafai.

Watu wanapokuwa katika msongo wa mawazo huwa wanaamini kwamba kila mtu hafai kabisa. Wanaona kila mtu ni mbaya.

Wanaamini kuwa kila mtu anawachukia, wanaamini kila mtu anawawazia mabaya, wanaamini hakuna mtu anayewapenda, wanaamini hawawezi kusameheka.

Wao mara zote wanadhani kila mtu anakusudia hila dhidi yao. Kifupi sio watu wenye imani na mtu yeyote.

Si kweli kwamba kila mtu hakutaki, kuna watu bado wanakupenda na kukujali sana.

Usifike mahali ukaona kwa sababu ya mazingira unayopitia hauna thamani tena.

Hata kama kuna watu walikutamkia kwamba wewe hauna maana na haufai.

Ile kwamba hauwafai wao haimaanishi haumfai kila mtu.

Kuna watu wanakuona lulu ya thamani sana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment