Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Jua Kipaji Chako Kimebeba THAMANI Gani
ii. Kipaji Chako Kinalindwa Namna Gani?
iii. Kipaji chako ni kwa ajili ya watu gani?
iv. Kipaji Chako Kinajitofautishaje
v. Kipaji chako Kimeambatana na Hatari Gani
Katika Makala Hii Tutazungumzia Nguzo ya Pili
– Kipaji Chako Kinalindwa Namna Gani?
Kila kipaji lazima kilindwe ili kiweze kuwa na ufanisi na kitoe matokeo makubwa na pia kiishi kwa muda mrefu zaidi.
Kama unataka kufanikiwa kukifanya kipaji chako kizalishe thamani ya kifedha ni lazima ujue mambo yanayohitajika kufanyika ili kukilinda.
Kuna watu ambao waliwahi kuibuka wakiwa na vipaji vikubwa sana ila hawakuweza kudumu kwa muda mrefu kwa sababu walishindwa kuvilinda vipaji vyao.
Ukiwa na kipaji ila ukashindwa kukilinda basi kinaweza kisikupe faida ama kikakupa faida ya muda mfupi sana.
Kwenye kulinda kipaji chako ni lazima ujue kuhusu “Do’s and Don’t’s” (Mambo unayopaswa kuyafanya na yale usiyopaswa kuyafanya).
Kubeba kipaji chako na kukifanya kilete matunda hakuna tofauti kabisa na mama ambaye ni mjamzito, kuna masharti anatakiwa ayafuate sio kwa sababu yake yeye ila kwa sababu ya usalama wa mtoto aliyeko tumboni kwake.
Kuna mambo lazima ujizuie kuyafanya na mengine ujilazimishe kuyafanya ili kukifanya kipaji chako kidumu na kilete matokeo.
Ukiwa na kipaji na ukaishi maisha yasiyo na nidhamu uwe na uhakika kipaji chako hakitaleta matokeo, kitaleta matokeo kidogo, ama kitaleta matokeo kidogo sana au hakitadumu muda mrefu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.