Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. WapendaMzuka (Thrill Seeker)
ii. Wanaoendeshwa na Maoni ya Watu
iii. Wanaoogopa Kulipia Gharama ya Maamuzi Yao
iv. Wanaosubiri Ukamilifu wa Jambo
v. Wanaojirundikia Mambo Mengi Pasipokuwa na Umuhimu (Busy Procrastinators)
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Nne
– Wanaosubiri Ukamilifu wa Jambo
Umeshawahi kukutana na watu ambao huwa wanaitwa “Perfectionist”?
Hawa ni watu ambao huwa kitu pekee kinachowafanya waghairishe kufanya jambo fulani ni kwa sababu huwa wanasubiria mazingira kamilifu ya kile ambacho wanataka kukifanya katika maisha yao.
Hawa ndio watu ambao huwa hawaanzi kufanya kitu chochote hadi waone mazingiria yote yako sawa kabisa na hakuna uwezekano wa kufeli.
Hawa ndio wale kila unapowauliza kwa nini hawajaanza kulima, kufanya biashara, kutekeleza wazo lao la muda mrefu basi jibu lao la kwanza huwa, bado nasubiria mambo yawe sawa.
Ukifuatilia wafanyabiashara na watu wengi waliofanikiwa katika maisha sifa yao mojawapo ni kuwa tayari kuanza hata kama mazingira bado hayajawa kamilifu kwa asilimia 100.
Ukweli wa mambo ni kuwa, hakuna siku yoyote katika maisha yako ambapo kila kitu kitakuwa kiko sawa kwa asilimia 100 kama ambavyo unataka, hivyo kusubiria kuwa na mazingira timilifu ni kujichelewesha.
Unatakiwa uwe tayari kuanza kufanya angalau unapokuwa na mazingira ya kujitosheleza kidogo kuanza hata kama hayajawa bado kamilifu kama ambavyo unataka.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.