Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ii. Neno La Mungu
iii. Maombi Yako Binafsi
iv. Kufunga
v. Kuwa Chini Ya Uongozi Wa Kiroho
Katika Makala Hii Tutazungumzia Nguzo Ya Tatu
– Maombi Yako Binafsi
Kazi kubwa ya maombi sio kukusaidia kupata vitu unavyovihitaji kutoka kwa Mungu, bali ni kukusaidia kuendelea KUFANANA katika ASILI na Mungu unayemuomba.
Kazi ya maombi ni KUKUBADILISHA ili ufanane na unayemuomba KIMAMLAKA na KIUTENDAJI.
Ndio maana YESU na MUSA walipotumia muda mwingi kwenye maombi, matokeo ya maombi yao yalikuwa ni KUBADILISHWA wanavyoonekana hadi wanadamu wenzao wakawaogopa (Mark 9:2-5, Mwanzo 34:2930).
Kadiri unavyoendelea kukaa kwenye maombi, ndivyo unavyozidi kufanana na Mungu na ndivyo wanadamu wa kawaida wanavyozidi kukuogopa na kukuhofia.
Kazi nyingine ya maombi ni kukuhamisha ulimwengu, ndio maana YESU alipoomba kulikuwa na viumbe wasiokuwa na mwili wa nyama wakamtokea (MUSA na ELIA);
maombi yanakusaidia kupata “access” ya ulimwengu wa roho na kuhusiana na viumbe wa rohoni (Malaika n.k) ambao wanaweza kukusaidia kazi huku duniani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.