Iran yafanya uharibifu mkubwa nchini Israeli

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Baada ya siku kadhaa za mashambulizi yake bila mafanikio makubwa, Iran imeweza kusababisha uharibifu mkubwa nchini Israeli, baada ya makombora yake kupenya ngome za anga za nchi hiyo, na kugonga maeneo kadhaa.

Nguvu ya mashambulio ya Iran ilikuwa imepungua, ikionekana kuwa dalili ya mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya jeshi la Iran.

Serikali ya Israel ilikuwa imetangaza kulegeza masharti kutokana na baadhi ya vikwazo vilivyowekwa kwa sababu ya vita.

Mashambulizi ya asubuhi ya leo, yanaonyesha kuwa Iran bado ina uwezo wa kurusha makombora na kusababisha madhara.

Maeneo yaliyopigwa ni pamoja na Kituo cha Matibabu cha Soroka katika mji wa kusini wa Beersheba, Holon, ambapo kombora lilitua kati ya majengo, na Ramat Gan, yote katika mji wa Tel Aviv.

Iran ilisema lengo huko Beersheba ni kile ilichosema kuwa ni shabaha ya kijeshi karibu na hospitali hiyo lakini Sharren Haskel, naibu waziri wa maswala ya kigeni wa Israel, aliishutumu Iran kwa kuilenga hospitali ya Soroka kimakusudi.

Haijabainika ni malengo gani yalioshambuliwa katika miji mingine iliyoathiriwa.

Iran imekuwa ikijibu takriban wiki moja ya mashambulizi ya anga ya Israel kwenye maeneo ya kijeshi na nyuklia, vituo vya nishati, viwanja vya ndege, majengo ya serikali na pia maeneo ya makazi.

Iran inasema hivi ni vita vya uchokozi, na kwamba ina haki ya kujilinda.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment