Marekani imerejelea maombi ya viza za wanafunzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Utawala wa Rais Donald Trump Jumatano 18/06/2025 uliamuru kurejelewa kwa miadi ya viza za wanafunzi lakini utaimarisha kwa kiasi kikubwa uhakiki wake kwenye mitandao ya kijamii ili kubaini waombaji wowote ambao wanaweza kuwa na chuki dhidi ya Marekani, kulingana na taarifa za Wizara ya Mambo ya nje iliyopitiwa na Reuters.

Maafisa wa ubalozi wa Marekani sasa wanatakiwa kufanya “uhakiki wa kina” wa wanafunzi wote na waombaji viza kutoka nchi za kigeni ili kubaini wale “wenye mitazamo ya chuki dhidi ya raia wetu, tamaduni, serikali, taasisi, au kanuni za msingi za Marekani,” ilisema taarifa hiyo ya tarehe 18 Juni na kutumwa kwa balozi za Marekani.

Maafisa pia wanashauriwa kuwa macho wakati wanafanya uchunguzi wao kwa “utetezi wowote, wa misaada au msaada kwa magaidi wa kigeni na vitisho vingine kwa usalama wa kitaifa wa Marekani,…uungaji mkono wa unyanyasaji au dhuluma dhidi ya Wayahudi, “na kuwabaini” waombaji ambao wanaonyesha historia ya harakati za kisiasa “na kuzingatia” uwezekano wa kuendeleza shughuli kama hizo huko Marekani. “

Inaonekana kwamba upanuzi wa uchunguzi huu unakusudiwa kuwa zaidi ya kwenye mitandao ya kijamii hadi aina yoyote ya uwepo wa chochote mitandaoni, pamoja na machapisho na ujumuishaji katika hifadhidata za mitandaoni.

Vile vile, waombaji viza wameamriwa kuwezesha akaunti zao za mitandao ya kijamii kuweza kufikiwa na “kila mmoja” kusaidia uchunguzi wa ziada.

Maafisa wanahitajika kupiga picha na kuhifadhi chochote chenye kuzua wasiwasi na kuweka kwenye rekodi zao.

Wizara husika imesema kuwa kuanzia sasa uchunguzi wa aina hii utakuwa lazima kwa waombaji wapya na wanaoomba viza kwa mara nyingine.

Mei 27, utawala wa Trump uliamuru balozi zake nje ya nchi kuacha kupanga miadi mipya ya waombaji wa viza za wanafunzi ikisema wizara ya mambo ya nje ilikuwa inajipanga kupanua mchakato wa uchunguzi kwa wanafunzi wanaoomba viza hadi katika mitandao ya kijamii.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment