Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maafisa wawili wa polisi waliomshambulia na mmoja wao kumfyatulia risasi mchuuzi wa barakoa wataendelea kuzuiliwa na polisi kwa siku 15 zaidi huku uchunguzi ukiendelea.
Klinzy Masinde Barasa na Duncan Kiprono watazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Capitol Hill ili kuruhusu upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi wake.
Maafisa hao walikamatwa baada ya vídeo ya wawili hao kumpiga na mmoja wao kumfyatulia risasi kwa karibu Boniface Kariuki wakati akijaribu kuondoka kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya kijana Albert Ojwang aliyekufa akiwa kizuizini.
Wakati huo huo, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat anatarajiwa kufika mbele ya Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) leo Alhamisi kurekodi taarifa kuhusu kifo cha mwanablogu Albert Ojwang.
Kifo cha kutatanisha cha mwanablogu huyo kimesababisha maandamano katika maeneo mbalimbali nchini Kenya huku kukiwa na shinikizo la kuwataka waliohusika na mauaji hayo katika ngazi za juu za idara ya polisi nchini Kenya wajibishwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.