Watu wanakutazama na kukutathmini kulingana na wao walivyo

Mungu anajua faida ya kutokutupa vitu tunavyovitamani, kwa sababu vinaweza kuwa NA hasara ya muda mrefu na maumivu makali sana.

Je! Utachagua kipi kati ya kupata na kufurahia kitu kwa muda mfupi kisha kikawa cha majuto kwako? Au kutopata unachotaka ukaumia lakini ukawa umeokolewa na hasara mbaya zaidi ambayo ingekupata miaka yote? “TAFAKARI” Zaburi 106:14-15
Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani.
Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao.
Watu wanakutazama na kukutathmini kulingana na wao walivyo, ndio maana si ajabu wakakuhusisha na mambo ya kushindwa sio kwa sababu umeshindwa ila ni kwa sababu hawajawahi kushinda na hawaamini kuna mtu anaweza kushinda.

Ila Mungu anakutazama vile ulivyo, ndio maana anataka ushinde zaidi ya vile unavyoamini una nguvu ya kushinda. MTAZAMO WA MUNGU KUHUSU WEWE NI KUKUPATIA AMANI NA ANAKUWAZIA MEMA. Acha kuumizwa na mtazamo wa watu juu yako.

WATU HUVIONA VITU SI KAMA VILIVYO BALI WAO WALIVYO.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment