Walioshitakiwa kwa shambulio la ugaidi la Dusit D2 wahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.
Maelezo ya picha,Washambuliaji wawili walioonekana hapa walipokuwa wakiingia

Mahakama ya kupambana na ugaidi nchini kenya imemhukumu mwalimu wa madrassa mwenye umri wa miaka 61 kifungo cha miaka 30 kwa kusababisha shambulio la kigaidi katika jengo la hoteli la Dusit D2 mjini Nairobi.

Mohamed Abdi Ali alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kila moja ya mashtaka 14 kwa kuwezesha kitendo cha kigaidi kinyume na Kifungu cha 9A cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ambayo itakwenda sambasamba na kifungo cha ziada cha miaka 15 kwa mashtaka ya Njama ya kufanya kosa kinyume na Kifungu cha 23 (2) kama inavyosomwa na 23 (4) ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2012.

Mahakama pia ilimhukumu Hussein Mohamed Abdille Ali mwenye umri wa miaka 22 kutumikia kifungo cha miaka 15 baada ya kuhukumiwa kwa kosa la Njama ya kufanya uhalifu na miaka mingine 15 kwa kuwezesha kitendo cha kigaidi chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Adhabu hizo za vifungo zitatekelezwa kwa pamoja.

Watu hao wawili walishitakiwa kwa kufanya shambulio la kigaidi la Januari 15, 2019, katika Jengo la Hoteli la Dusit D2 mjini Nairobi, ambalo liliua watu 21, wakiwemo raia wa kigeni, na kuwaacha wengine kadhaa wakiwa na majeraha ya kutishia maisha.

Alipokuwa akitoa hukumu yake Alhamisi, Jaji Diana Kavedza alisema mahakama imeridhika kwamba mashtaka yamethibitisha pasi na shaka kuwa Hussein Mohamed Abdille na Mohamed Abdi Ali wamehusika na shambulio hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment