Mahitaji Matano Utakayotaka Kuhudumia…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. The Drive to Bond (Kuunganika na Watu)

ii. The Drive to Acquire (Kupata na Kumiliki)

iii.The Drive to Learn (Kujifunza

iv. The Drive to Defend (Kujilinda

v. The Drive to Feel (Kuridhisha Hisia)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Hitaji La Nne

– The Drive to Defend (Kujilinda)

Kila mwanadamu huwa anapenda kujihakikishia kuwa yuko salama kila wakati, na hivyo moja ya haja kubwa aliyonayo kila mtu duniani ni kujilinda na mambo mbalimbali ambayo yanahatarisha usalama wake.

Haja hii ya watu kutaka kujilinda, huwa inatengeneza fursa nyingi sana za kibiashara ambazo wewe unaweza kuamua kuzitumia.

Baadhi ya watu ambao wanafanya biashara katika eneo hili ni pamoja na watu wanaendesha kampuni za ulinzi ili kuwasaidia watu kujilinda na madhara ya kimwili.

Wapo pia ambao wanatoa huduma za bima za afya ili kuwahakikishia watu kuwa watakuwa salama pale madhara ya kiafya yatakapotokea na wapo ambao wanatoa huduma za kisheria ili kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama wanapopata matatizo ya kisheria.

Huduma hizi na nyingine nyingi, huwa zinalenga kumsaidia mtu kupata uhakika kuwa yuko salama.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment