Khamenei: ‘Wairani sio wale wanaojisalimisha’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amejibu mashambulizi ya Israel kwenye taarifa iliyosomwa na mwanahabari kupitia chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali.

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema kwamba “watu wenye hekima wanaoifahamu Iran, watu wake na historia yake kamwe hawazungumzi na taifa hili kwa lugha ya vitisho, kwa sababu Wairani sio wale wanaosalimu amri”.

Kiongozi huyo wa Iran alisema kuwa hatua ya kijeshi ya Marekani itakabiliwa vilivyo.

“Aina yoyote ya uingiliaji kijeshi wa Marekani bila shaka itakabiliwa nam atokeo mabaya,” ilisema taarifa ya Khamenei.

Wakati huo huo,Waziri wa mambo ya nje wa Israel amesema kushambulia Iran ni hatua ya mwisho kabisa katika barua kwa Umoja wa Mataifa.

Waziri Gideon Sa’ar ameelezea sababu ya Israel kuanzisha mashambulizi yake dhidi ya Iran wiki iliyopita katika barua ambayo aliituma kwa mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

Anadai kuwa nchi hiyo haikuwa na chaguo baada ya “miongo kadhaa” ya “vitendo vya kisiri vya uadui” vya Iran na vitisho vya viongozi wake “kuangamiza” Israel.

“Siyo matamshi tu. Iran ina mpango mkakati wa kuiondoa Israel, ambayo inajumuisha mipango na hatua madhubuti kufikia lengo hili,” Sa’ar aliandika.

Pia alisema Israel ilifanya shambulizi mara ya kwanza katika kile kilichokuwa “ni wakati muafaka” kuchukua hatua kuzuia shambulio la baadaye la Iran.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment