Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Familia ya aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Lungu imesitisha kurejeshwa kwa mwili wake kutoka Afrika Kusini, ikiishutumu serikali kwa kukiuka makubaliano muhimu kuhusu mazishi yake.
Mipango hiyo ilikuwa imekamilika na mwili wake ulipaswa kurejeshwa nyumbani Jumatano kwa ndege ya kibinafsi ya kukodi baada ya siku kadhaa za kutokuwa na uhakika na mazungumzo kati ya familia na serikali.
Lakini familia hiyo sasa imesitisha mpango huo, ikisema “inapata ugumu sana kuamini kwamba serikali itadumisha makubaliano waliofikiana hadi mwisho”.
“Cha kusikitisha ni kwamba mwili wa Rais Edgar Chagwa Lungu hautarejea leo,” msemaji wa familia Makebi Zulu alisema Jumatano.
Bw Zulu alisema serikali ilitoa rasimu ya mpango wa mazishi, bila kushauriana na familia.
Rais Hakainde Hichilema alipangiwa kuupokea mwili huo utakapowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu, Lusaka.
Mwili wa rais huyo wa zamani ulitarajiwa kupelekwa katika makazi yake mjini Lusaka ambako ungelala kabla ya kuagwa kitaifa tarehe 22 Juni na kuzikwa siku iliyofuata.
Katika hotuba siku ya Jumatano, Bw Zulu alisema serikali imebadilisha mpango uliokubaliwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.