Marekani na Iran: Malumbano ya Trump na Khamenei kwenye mitandao ya kijamii

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Huku Israel na Iran zimekuwa zikirushiana makombora katika siku za hivi karibuni, Raisi wa Marekani Donald Trump na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei wamekuwa wakijibizana kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi ndizo kauli zao za hivi punde zaidi kwa kipindi cha saa 24 zilizopita:

Mapema Jumanne, Trump alitumia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kudai “udhibiti kamili wa anga juu ya Iran”.

Aliendelea kumtahadharisha Khamenei: “Tunajua hasa ni wapi yule anayeitwa ‘Kiongozi Mkuu’ amejificha. Yeye ni shabaha rahisi, lakini yuko salama huko – Hatutamtoa (kuua!), angalau sio kwa sasa.”

Alisisitiza kuwa: “uvumilivu wetu umepungua”, Trump alionya katika ujumbe wake wa mwisho: “MUJISALIMISHA BILA MASHARTI!”

Hakuna dalili za hilo kwa kadiri Tehran inavyohusika.

Katika mfululizo wa machapisho kwenye X, katika akaunti tofauti za lugha, Khamenei alisema Iran “haitafanya maelewano kamwe na Wazayuni”.

“Hatutawaonea huruma Wazayuni,” tafsiri ya chapisho hilo inasomeka. Katika chapisho tofauti, anasema “vita vinaanza”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment