Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Angalia Kitu Unachokipenda Sana
ii. Kagua Ujuzi Wako
iii. Mahitaji Ya Usimamizi
iv. Uingiaji na Utokaji wa Fedha Kwenye Biashara
v. Uendelevu wa Wazo
vi. Uwezekano wa Kukua Kwa Biashara
vii. Kipaji Chako
Katika Makala Hii Tutazungumzia Kigezo Cha Sita
– Uwezekano wa Kukua Kwa Biashara
Ili uone faida ya biashara unayoifanya, ni lazima pia uwe na uwezo wa kuikuza zaidi ili kuongeza mauzo yako ya kila siku.
Unapochagua biashara ya kufanya, ni muhimu kufanya tathimini ya namna inavyoweza kukua.
Kabla haujaanza kufanya biashara yoyote ile, hebu jiulize: Hivi uwezekano wa biashara hii kukua ukoje?
Eneo la kwanza la kukua kwa biashara yako ni uwezo wako wa kuhudumia wateja wengi zaidi.
Ukiona biashara unayoichagua ina uwezo wa kupanuka na kuwafikia watu wengi zaidi, inamaanisha unaweza kuikuza na ikakupa uhakika mkubwa zaidi wa kipato.
Ila kama ukiona aina hiyo ya biashara ni ngumu kuikuza kwa kuwafikia watu wengi zaidi, inamaanisha itakupa changamoto kubwa sana huko mbeleni.
Jambo lingine unalotakiwa kuangalia ni uwezo wa kudurufu biashara yako (duplicate)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.