Damu ya Yesu ikufunike na kufuta kila laana

Unapokuwa unaomba lazima ujue unaiomba nguvu ya aina gani na inauwezo wa kufungua nini,kufanya maombi bila kuwa na Imani kwa Mungu wala matumaini ni kupoteza Muda,kutokuwa na na Imani na Damu ya Yesu iliyomwagika msalabani kwaajiri ya ukombozi wa ulimwengu ni kupoteza muda pia wakati wa maombi yako,cha kufahamu ni kwamba damu ya Yesu ina uwezo wa kumpa anayeomba kwa imani chochote anacho taka,na kufungua kila aina ya vifungo,Damu hiyo ina nguvu ya kukutenga mbali na kila aina ya uchawi ukijua kuitumia wala hauta teseka tena.

Damu ya Yesu ikufunike na kufuta kila laana na roho za mafatilizi kwenye maisha yako katika Jina la Yesu.

Kuna watu wanaishi duniani hawaja pata neema ya kumjua Mungu lkn wana mali na uwezo mkubwa kwenye maisha yao,Mungu huwatumia hao hao kukubariki wewe unaeomba baraka mbele zake,Leo Mungu akawaguse wabadili maisha yako wakakupe mali na utajiri sawa sawa na neno lake Isaya 60:11 katika Jina la Yesu POKEA KWA IMANI


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment