Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vikosi vya Israel vimewauwa zaidi ya Wapalestina 51 na kujeruhi wengine wengi zaidi baada ya kufyatua risasi karibu na eneo la kusambaza misaada kusini mwa Gaza, walioshuhudia na waokoaji wanasema.
Shirika la ulinzi wa raia linaloendeshwa na Hamas limesema kuwa wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi watu waliokuwa karibu na eneo la misaada huko Khan Younis. Zaidi ya watu 200 waliripotiwa kujeruhiwa.
Jeshi la Israel limesema kuwa linachunguza ripoti hizo.
Ni matukio ya hivi punde zaidi, na yanayoweza kuwa mabaya zaidi, ya karibu kila siku ya ufyatuaji risasi ambayo yamekuwa yakitokea hivi karibuni karibu na maeneo ya usambazaji wa misaada huko Gaza.
Siku ya Jumatatu, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk alisema Israel ilikuwa ikitumia chakula kama silaha na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu ufyatuaji risasi karibu na maeneo ya kutoa misaada.
Akihutubia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu, alisema: “Njia na mbinu za vita za Israel zinawasababishia Wapalestina katika Gaza mateso ya kutisha na yasiyo kifani.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.