Usipoteze Focus Yako.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Njia Mojawapo Rahisi Sana Ya Mtu Kukufelisha Kwenye Maisha Yako Ni Kukupotezea “FOCUS”…

Yaani anakutoa kwenye mstari.

Mara nyingi, ni ngumu sana kujua Kama unatolewa kwenye mstari.

Hadi pale madhara yanapoanza kuonekana.

Hii ni kwa sababu baadhi ya mambo yatakayokutoa kwenye mstari…

…yataonekana ni mazuri kwa nje.

Kuna wale watakutoa kwenye mstari kwa kukupa fursa nzuri.

Ila fursa ambayo sio sahihi kwako.

Yaani kuna vitu ambavyo hata wewe ndani ya moyo wako unajua sio sahihi kuvifanya.

Ila kwa sababu fursa imetokea, basi unaamua kuvifanya.

Mwisho wa siku vinakupeleka usipotarajia.

Wengine watakutoa kwenye “FOCUS” kwa kukuweka bize sana na mambo mengi yasiyo na faida.

Yaani, unajikuta uko bize kila siku na kila wakati ila Matokeo hakuna.

Jitahidi sana kuilinda “FOCUS” yako.

Yaani jikite kwenye kufanya vitu vya muhimu tu.

Vitu vinavyokusaidia kusogea kwenye malengo yako makubwa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment