Mambo 7 Muhimu Ya Kuyaepuka Baada Ya Kuachana…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kutafuta Mtu Mbadala Kwa Haraka Kabla Moyo Haujapona
ii. Kufanya Mambo Ili Umuoneshe Kuwa Unaendelea Vizuri
iii. Kuchukia Kila Mtu Hata Wasiohusika
iv. Kufanya Mbinu Za Kumdhuru
v. Kuhitimisha Hautapata Mtu Mwingine Kama Yeye
vi. Kujingiza Kwenye Tabia Hatarishi Ili Kupoteza Mawazo
vii. Kujiondolea Thamani

Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo la Sita

– Kujingiza Kwenye Tabia Hatarishi Ili Kupoteza Mawazo

Katika hali ya kutafuta uponyaji wa moyo, wako watu wengi sana ambao wamejiingiza kwenye tabia hatarishi zilizowaharibu zaidi.

Moyo unapokuwa “empty”, huwa unatafuta kitu cha kujazia.

Katika harakati hizi, unaweza kujikuta umeanza kufanya vitu ambavyo vinakuharibu zaidi badala ya kukusaidia.

Kuna watu ambao wanajiingiza kwenye tabia za unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara/madawa na hata kuingia kwenye uraibu wa kuangalia picha za ngono.

Wapo ambao baada ya kuachana na mtu waliyempenda, wamejikuta wanajiingiza kwenye “umalaya” wa kulala na kila mtu kama njia ya kujifariji.

Tabia hizi zote, badala ya kukusaidia, zitakuingiza zaidi kwenye changamoto kubwa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment