Sababu 6 Kubwa Zinazoleta Maumivu Sana Baada Ya Kuachana…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Hisia Za Kufeli.
ii. Mabadiliko Ya Maisha Yako Ya Kila Siku.
iii. Kubadilika Kwa Mahusiano Na Watu Wengine.
iv. Uwekezaji Uliouweka Hapo Kabla.
v. Mabadiliko Ya Mipango Na Malengo Yako.
vi. Aibu Kwa Jamii Inayowafahamu.

Katika Makala Hii Tutazungumzia Sababu ya Tano

– Mabadiliko Ya Mipango Na Malengo Yako.

Kila mtu ambaye unakuwa nae kwenye mahusiano, kuna mipango ambayo unakuwa nayo unayotamani kufanikisha nae.

Kuna mwingine mlipanga mahali pa kuishi na mlianza kufanya ujenzi, kuna mwingine ulipanga ndiye atakuwa mbia wako wa biashara wa kudumu, ulimwambia siri nyingi binafsi na kazi zako n.k

Mnapoachana lazima itakuvuruga. Hapa inakuwa sio tu kumpoteza yeye, bali pia kuharibika kwa mipango ambayo mlipanga pamoja ikiwemo ile uliyomuambia tayari na mingine ambayo ulikuwa bado haujamuambia.

Kuna wakati unapoachana na mtu kulingana na hatua ambayo mmefikia inakuwa kama vile unaanza upya maisha yako.

Kuna wengine wanapoachana inabidi wagawane vitu, watoto au hata kulazimika kuhama walipokuwa wanaishi.

Hii yote inakusababishia kuanza chini zaidi kuliko pale ulipokuwa.

Haya yote yatakusababishia maumivu makali sana.

Hapo baadae tutajifunza cha kufanya kama kuachana kwako kumekuvurugia mipango yako ya awali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment