Kenya: Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat ajiondoa kupisha uchunguzi

.

Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat amejiondoa kupisha uchunguzi unaoendelea kwa sababu ya kifo cha Albert Ojwang, mwanablogu aliyekufa mikononi mwa polisi.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Juni 16, 2025, Lagat alisema amechukua hatua hiyo kwa nia njema kutokana na jukumu na wajibu alionao kwenye nafasi yake.

Lagat aliongeza kuwa majukumu yake yatatekelezwa na naibu wake hadi uchunguzi utakapokamilika.

Pia “natoa rambirambi zangu kwa familia ya Bwana Albert Ojwang kwa kumpoteza mpendwa wao,” taarifa hiyo ilisema.

Lagat aliahidi kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi.

Kifo cha Albert Ojwang, kimesababisha hasira miongoni mwa umma huku maafisa kadhaa waliokuwa kazini wakati huo wakikamatwa.

Uchunguzi huo unaendeshwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA).

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment