Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Israel limetoa “onyo la dharura” kwa watu “mara moja” kuondoka eneo la Tehran, mji mkuu wa Iran.
“Katika kipindi cha saa zijazo, IDF itafanya operesheni katika eneo hilo, kama ilivyofanya katika siku za hivi karibuni kote Tehran, kushambulia miundombinu ya kijeshi ya utawala wa Iran,” msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Avichay Adraee aliweka ujumbe huo kwenye mtandao wa X.
Ameambatanisha ramani kwenye maeneo yaliolengwa katika onyo hilo akisema watu katika sehemu za wilaya ya tatu ya jiji hilo wanapaswa kuondoka.
“Uwepo wako katika eneo hili unahatarisha maisha yako,” onyo hilo linaisha hapo.
Milipuko imesikika magharibi mwa Tehran
Tumesikia kutoka kwa watu wa magharibi mwa Tehran kwamba wamesikia milipuko mikubwa.
Video na picha zinazojitokeza kwenye mitandao ya kijamii ya Iran zinaonyesha moshi unaopanda katika milima iliyo karibu iliolengwa.
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa ulinzi wa anga wa mji huo umeanzishwa magharibi mwa Tehran, huku shirika la habari la Fars linaloshirikiana na IRGC likisema Israel imelenga kambi ya kijeshi katika eneo hilo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.