Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema aliipa Tehran nafasi baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano yalikuwa yanakaribia kuingia awamu ya sita Jumapili.
“Niliwaambia, kwa maneno makali, “fanyeni tu,” ingawa walijaribu sana, haijalishi walikuwa karibu vipi, hawakuweza kufanikiwa,” Trump anaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth.
“Iran lazima ifanye makubaliano na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Dola ya Iran. Hakuna kifo tena, hakuna uharibifu tena, FANYA TU, KABLA HAMJACHELEWA.”
Hapo awali Trump alisema anafahamu mipango ya Israel kabla ya kuanza mashambulizi usiku kucha, lakini aliweka wazi kuwa wanajeshi wa Marekani hawakushiriki katika operesheni hiyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.