Hatua 5 Ambazo Lazima Uzipitie Kabla Maumivu Ya Kuachana Hayajaisha…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

i. Denial (Kutokukubali Kuamini Kwamba Imetokea)

ii. Anger (Hasira)

iii. Bargaining (Kujaribu kutafuta muafaka)

iv. Depression (Msongo wa mawazo)

v. Acceptance (Kukubali matokeo)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Hatua Ya Pili

– Anger (Hasira)

Baada ya kuvuka changamoto ya kwanza inayohusiana na kukataa uhalisia, katika hatua hii mtu anakuwa tayari ameshapata uhakika kuwa jambo hili limetokea.

Pamoja na kwamba amekubaliana na hali iliyotokea anakuwa ni mtu mwenye hasira sana ikiwa kama njia ya kuonesha kutokuridhishwa na kitu ambacho kimetokea.

Kumbuka kuwa hasira ni udhihirisho na utambulisho (manifestation and expression) wa kutokuridhishwa na kitu fulani.

Hata hivyo katika hatua hii mtu huonesha hasira kwa njia kuu mbili: Moja ni huelekeza hasira zake kwake mwenyewe:

Hapa mtu anaanza kuonesha kutokujikubali, anakasirikia maamuzi yake ya kuanzisha hayo mahusiano, anajilaumu na anakasirika kwa sababu ya muda ambao anaona kama amepoteza kabisa.

Mara nyingi mtu akiwa kwenye hali hii utaanza kuona anaanza kuacha kujithamini.

Kama alikuwa mtanashati ama anajiremba vizuri ataanza kuacha kufanya hivyo kwani atahitimisha kuwa hakuna faida yoyote ile.

Akiwa amebakia peke yake anajiona hana thamani na anaanza kujiona kuwa ni mtu wa hovyo asiye na thamani.

Wengine wanapata hisia kuwa mtu aliyekuwa nae kwenye mahusiano alidhamiria kumpotezea muda na kumuumiza kwa makusudi, mawazo haya yote yanazidi kumpa hasira.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment