Maeneo 4 Muhimu Ya Kumpa Uongozi Mume Wako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Maamuzi Yanayohusu Mwelekeo Wako

ii. Maamuzi Yanayohusu Familia Yenu

iiii. Maamuzi Yanayohusu Watoto Wenu

iv. Maamuzi Yanayohusu Watu Muhimu Kwenu (Wazazi, Ndugu N.k)

Katika Makala Hii Tutazungumzia Eneo la Kwanza

– Maamuzi Yanayohusu Mwelekeo Wako

Mfanye mume wako ajihisi kuwa ni mtu wa kwanza kujua kuhusu mwelekeo wa maisha yako.

Hakikisha unampa taarifa ya unachowaza na unachopanga mapema.

Hii itamfanya kwanza ajisikie kuwa unamuamini na pili itamfanya ajisikie kuwajibika kwenye hicho ulichomuambia.

Kumbuka kuwa, hata kama hana uwezo wa kukusapoti kipesa, kwake inamuongezea ujasiri unapomuhusisha.

Usiache kazi tu bila yeye kujua, usimsumprise kwa kuanza kusoma bila yeye kufahamu n.k

Mshirikishe na kutaka ushauri wake kuhusu maamuzi yako ya kwenda kusoma mahali (ndani au nje ya nchi).

Mfanye aone amehusika kwenye kukupa mawazo na kufikia hitimisho ambalo ndio haswa litapelekea hatua utakazochukua.

Ukifanya mambo bila kumshirikisha unampa ujumbe kuwa yeye si muhimu kwenye maisha yako na hivyo haukutarajia akusadie kwenye chochote kile.

Kuna wakati unaweza kuona kama kila unapomshirikisha huwa hasemi chochote kile, usipumbazike na hilo likakufanya uache kumwambia, niamini mimi, huwa anathamini na usiache kumwambia.

Ukitaka kujua kuwa anathamini, siku utakapoacha kumshirikisha ndio utaona “reaction” yake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment