Trump asema makubaliano ya madini adimu ulimwenguni ‘yafikiwa’ na China

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mazungumzo yanayolenga kupunguza mvutano kati ya Marekani na China yamemalizika kwa “makubaliano”, kulingana na Rais wa Marekani Donald Trump.

Alisema China imekubali kuuzia makampuni ya Marekani sumaku na madini adimu duniani, huku Marekani ikipuuzilia mbali vitisho vyake vya kufuta viza za wanafunzi wa China.

“Mkataba wetu na China umekamilika, kilichosalia ni idhini ya mwisho kutoka kwa Rais Xi na mimi,” Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social.

Tangazo hilo lilifuatia siku mbili za mazungumzo ya kina mjini London kusuluhisha mizozo iliyoibuka tangu pande hizo mbili zilipoafikiana makubaliano ya awali, mnamo mwezi wa Mei, baada ya ushuru wa forodha ulioongozwa kukaribia kulemaza biashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment