Makosa 4 Wanayofanya Wanawake Wenye Uwezo Mkubwa Wanapokuwa Ndani Ya Ndoa…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. umnyang’anya Mwanaume Nafasi Yake Ya Uongozi Kwenye Maisha Yako.

ii. Kushindana Na Mwanaume.

iii. Kumpa Nafasi Mwanaume Mwingine Kuwa Na Sauti Kwenye Maisha Yako Kuliko Mwanaume Wako

iv. Kupoteza Haiba Ya Kike

Katika Makala Hii Tutazungumzia Kosa La Kwanza

– umnyang’anya Mwanaume Nafasi Yake Ya Uongozi Kwenye Maisha Yako.

Kwa sababu ya mambo yote haya, huwa mkombozi wa familia anajikuta anaanza kubeba majukumu mazito sana akiwa na umri mdogo sana.

Kwa sababu mkombozi wa familia huwa anakuwa na moyo sana kusaidia ndugu zake na kwa namna fulani huwa anakuwa anajiweza kidogo kiuchumi, ni jambo la kawaida kabisa kuchukua baadhi ya ndugu zake na kukaa nao ili kuwasaidia.

Hata hivyo katika kufanya hivyo, huwa anakutana na changamoto nyingi sana zinazokatisha tamaa.

Moja ni pale mkombozi anapoamua kumsaidia ndugu mtaji, pengine wa biashara.

Kinachokuja kutokea ni kuwa, mtaji alioutoa huwa unapotea na hakuna kitu ambacho kitaendelea, yaani yule aliyesaidiwa anarudi chini anapoteza kila kitu na akiulizwa huwa hataki kuwajibika.

Katika mfumo wa kifamilia, mwanaume ameumbwa kuwa ni kiongozi.

Ingawa ni ukweli usiopingika kuwa, wapo wanaume ambao wamepoteza uwezo wao wa kiuongozi ila usisahau kuwa katika hali hiyo hiyo bado wanahitaji nafasi yao ya kuwa kiongozi iendelee kuwepo.

Uongozi maana yake ni kuonesha njia. Maana yake ni kuwa na sehemu katika maamuzi muhimu.

Mwanamke yeyote ambaye anataka kupewa sapoti na mume wake, ni lazima ahakikishe kuwa amempa nafasi ya uongozi, hata kwa lazima.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment